Pata taarifa kuu
UGANDA-ARDHI-MZOZO

Museveni aanzisha kampeni kwa minajili ya marekebisho ya Katiba

Nchini Uganda, jitihada za kurekebisha Katiba kuhusu ardhi ni mojawapo ya changamoto kubwa zinazotia wasiwasi nchini humo.

Kwa upande wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, marekebisho ya Katiba ni muhimu (picha ya zamani).
Kwa upande wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, marekebisho ya Katiba ni muhimu (picha ya zamani). ©Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Uganda inajaribu kurekebisha Katiba ili kuharakisha utaratibu wa manunuzi ya ardhi zinazohitajika kwa sera yake kuu ya kazi muhimu. Lakini vurugu katika maeneo kadhaa tayari zimeripotiwa kwa sababu taratibu za kuhamisha watu zilifanyika. Marekebisho hayo kwa sasa yanazuiwa na Wabunge. Ili kujaribu kushawishi wananchi kuhusu manufaa ya hatua hii, wiki hii rais Museveni ameandaa mdahalo kupitia redio mbalimbali nchini humo kuanzia siku ya Jumatatu Septemba 4 magharibi mwa Uganda.

Kama ilivyo kawaida, rais ameanza kuwatafsiri wananchi wake manufaa ya hatu hiyo ya serikali. Marekebisho ya Katiba ni muhimu, rais Museveni amesema, huku akijaribu kufafanua baadhi ya mambo. "Kuna kamati ambayo itakutana na kuamua ikiwa mtu huyo ametapeliwa au la katika ununuzi wa ardhi yake. Sio katika sheria ya sasa hivi. Hivyo basi watu wanaosema kuwa Katiba haipaswi kubadilishwa wanakosea. "

Rasimu ya marekebisho inaeleza hasa kwamba majadiliano juu ya bei ya kuuza yanapaswa kufanyika baada ya serikali kuchukua milki ya ardhi. Migogoro tayari imeripotiwa, hasa katika mkoa wa Hoima, ambapo kutajengwa sehemu ya mitambo ya mafuta. Museveni ameshutumu vyombo vya habari kuchochea vurugu hizo. "Wanahabari kwenye redio wanawatia uoga raia kwamba Uganda itatumbukia katika machafuko," rais Museveni amesema. Wanahabari wanapinga wale wanaotaka kupata ardhi. Hali hii inachochea migogoro ya ardhi. Ninaomba wanachama wa NRM kuamka na kukataa mambo haya. "

Kampeni dhidi ya marekebisho haya imezinduliwa na kurushwa kwenye Twitter ikiwa na hashtag #MylandMylife. Wengi wanaogopa kuwa katika marekebisho haya ya Katiba pia huenda kukaondolea kikomo cha umri wa rais na hivyo kumuwezesha Museveni kuwania tena katika uchaguzi wa mwaka 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.