Pata taarifa kuu

Burundi yaendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu

Miaka miwili sasa tangu kuanza kwa mzozo wa kisiasa nchini Burundi siku kama ya leo mwaka 2015, wakati rais Pierre Nkurunziza alipoamuwa kuwania muhula wa 3, vifo vya watu, unyanyasaji na kutoweka kwa wapinzani wa serikali vimeendelea kushuhudiwa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na Mashirika ya kiraia.

Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi, katika sherehe za uhuru wa Burundi, Julai 1, 2016.
Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi, katika sherehe za uhuru wa Burundi, Julai 1, 2016. Onesphore Nibigira/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya kisiasa chini ya mratibu Benjamin William Mkapa ambaye ni rais wa zamani wa Tanzania, yanaonekana kukwama.

Makamu wa rais wa Burundi Gaston Sindimwo anasema mzozo ulikwisha zamani, kuna amani na sasa ni muda wa kuijenga nchi hiyo.

Hata hivyo visaa vya mauaji na kutoweka kwa wapinzani wa serikali vinaendelea kushuhudiwa kila kukicha.

Machafuko nchini Burundi yamesababisha watu wengi kupoteza maisha na maelfu ya raia kuyahama makazi yao na kukimbilia nchi nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.