Pata taarifa kuu
UGANDA

Mwanaharakati nchini Uganda afunguliwa mashtaka kwa madai ya kumtusi rais Museveni

Mwanaharakati nchini Uganda Dokta Stella Nyanzi amefunguliwa mashitaka ya udhalalishaji na matumizi mabaya ya mtandao baada ya kuandika katika maelezo katika ukurasa wake wa facebook yanayoonekana kumdhalilisha rais Yoweri Museveni.

Mwanaharakati nchini Uganda Dokta Stella Nyanzi
Mwanaharakati nchini Uganda Dokta Stella Nyanzi Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Nyazi ambaye pia ni Mhadhiri na mtafiti katika Chuo Kikuu cha Makerere aliandika katika ukurasa wake wa facebook na kumfananisha rais Yoweri Museveni kama makalio, maandishi ambayo Mahakama imesema ni kumdhalalisha kiongozi wa nchi.

Nchini Uganda, ni kinyume cha sheria kutoa maneno ambayo ni ya kumdhalalisha rais wa nchi na kukiwa na ushahidi mhusika hufunguliwa mashitaka.

Akizungumza Mahakamani, mwaharakati huyo amesema hakubaliana na mashitaka hayo na kushtumu uongozi wa rais Museveni na kusisitiza kuwa hawezi kunyamazishwa na serikali ya rais Museveni.

Wanaharakati na wanasiasa wa upinzani nchini humo walifurika Mahakamani jijini Kampala na kushinikiza kuachiliwa huru kwa mwanaharakati huyu kupitia mitandao ya kijamii, #FreeStellaNyanzi baada ya kukamatwa kwake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hivi karibuni, mwanaharakati huyo ameikosoa serikali kupitia Waziri wa Elimu kwa kuanzisha mchakato wa kutoa taulo za hedhi au sodo kwa wanafunzi wa kike katika shule za serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.