Pata taarifa kuu
KENYA

Mahakama maalum ya kusikiliza kesi za ufisadi yazinduliwa nchini Kenya

Mahakama maalum ya kusikiliza kesi zinazohusu tuhma za ufisaidi nchini Kenya, imezinduliwa rasmi jijini Nairobi.

Jengo la Mahakama jijini Nairobi
Jengo la Mahakama jijini Nairobi /www.ebru.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Jaji Mkuu nchini humo David Maraga amesema Mahakama hiyo maalum imetengewa kitengo maalum katika Mahakama kuu na inaanza kazi mara moja kushughulikia kesi mbalimbali za ufisadi.

Aidha, amesema lengo kuu la Mahakama hii maalum ni kusikilizwa kwa haraka kwa kesi hizo na hukumu kutolewa, ili haki itendeke kwa wale wanaotuhumiwa kufanya makosa ya kiuchumi nchini Kenya.

Hata hivyo, Jaji Mkuu amesema kuwa Mahakama hiyo itafanikiwa tu ikiwa kila mmoja atashirikiana na Mahakama hiyo yenye makao yake jijini Nairobi.

“Ikiwa hatutapata ushirikiano kutoka kwa kiongozi wa mashtaka ya Umma au hata Tume ya kupambana na ufisadi sisi kama Mahakama tutawaambia wananchi ukweli kuhusu kinachoendelea,” amesema Jaji Mkuu Maraga.

"Tutawaambia kuwa  mikono yetu imefungwa na tumefika mwisho,".

Maraga ambaye pia ni rais wa Mahakama ya Juu nchini humo amesema, idara yake haikuwa na lingine bali kuanzisha Mahakama hii ili kushughulikia kiwango kikubwa cha ufisadi nchini Kenya.

“Tumefikia uamuzi huu kwa sababu ya kiwango kikubwa cha ufisadi katika nchi yetu,” aliongeza Jaji Maraga.

Majaji watakaokuwa katika Mahakama hii, hawatatakiwa kusikiliza kesi zingine kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Mahakama nchini humo.

Uzinduzi wa Mahakama hii maalum umekuja baada ya raia wengi wa Kenya kuilalamikia serikali ya rais Uhuru Kenyatta kushindwa kupambana na ufisadi kutokana na kashfa mbalimbali za kupotea kwa fedha za umma.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.