Pata taarifa kuu
KENYA

Mahakama ya juu ya Kenya yasema rais mteule Uhuru Kenyatta alishinda kihalali

Mahakama ya juu nchini Kenya imetupilia mbali madai ya kupinga ushindi wa rais mteule uhuru kenyatta yaliyowasilishwa na vyama vya kijamii sambamba na muungano wa CORD, na kutangaza kuwa Uhuru Kenyatta alishinda kihalali. 

Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Akitoa maamuzi hayo Jaji mkuu Willy Mutunga amesema kuwa uchaguzi huo wa Machi nne ulifanyika kwa uhuru, uwazi na haki na kwamba uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.

Waziri mkuu Raila ambaye aliwasilisha madai ya kupinga ushindi wa Kenyatta hata hivyo ameridhia uamuzi wa mahakama na kukubali Uhuru Kenyatta kutawazwa kuwa rais wa nne wa taifa la Kenya.

Rais mteule Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto wataapishwa rasmi mnamo tarehe 9 mwezi April mwaka 2013, huku pia sababu za uamuzi wa mahakama ya juu kutupilia pingamizi dhidi ya Kenyatta kutolewa baada ya majuma mawili.

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.