Pata taarifa kuu

Kenya kudhibiti ajali barabarani watu 1213 wakiwa wamepoteza maisha mwaka huu

Katika kipindi cha miaka mitatu ,nchi ya Kenya imeshuhudia ongezeko la ajali na vifo barabarani

Ajali za barabara husababisha vifo vingi ya watu wenye umri kati ya miaka mitano na 29 kwa mujibu wa WHO
Ajali za barabara husababisha vifo vingi ya watu wenye umri kati ya miaka mitano na 29 kwa mujibu wa WHO AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Kenya William Ruto ,amezindua mpango kazi wa mamlaka wa usalama barabarani ,utakaosaidia kudhibiti visa vya ajali ambavyo vimezidi kuongezeka ,hii ikijiri wakati raia 1,213 wakiwa wamepoteza maisha katika kipindi kati ya Januari hadi sasa ,asilimia kubwa ya ajali hizo ikisababishwa na utepetevu wa madereva na tabia zembe za watumizi wa barabara.

Mpango huo wa miaka mitano unalenga kukumbatia mfumo unaoainisha mikakati ya usalama kati ya asasi zote husika .

Soma piaNini sababu za ongezeko la ajali nchini Kenya na takwimu zinasemaje

Ripoti ya halmashauri ya usalama barabarani ,National Transport Safety Authority ,imesema asilimia 80 ya ajali za barabarani nchini Kenya zinasababishwa na tabia za watumizi wa barabara haswa madereva ,ajali hizo zikiwa zinaweza kuzuilika.

Msimu wa Pasaka umeshuhudia idadi kubwa ya ajali ,madereva wengi wakiwa  wanaendesha kwa kasi ,kuendesha wakiwa walevi na kuwa na msongo wa mawazo.

Soma piaWatu 10 wamefariki katika ajali ya barabarani nchini Kenya

Rais Ruto amesema baadhi ya hatua maksusi za kukabilia hali hii ni faini za hapo kwa hapo zitatozwa wavunjaji sheria za barabara

Kwa mujibu wa takwimu za benki ya dunia,ajali za barabara hugharimu asilimia tano ya mapato ya taifa.

Carol Korir- RFI-Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.