Pata taarifa kuu

Uingereza na Rwanda kuaanza kutekeleza mpango wa kusafirishwa wahamiaji

Nairobi – Rais wa Rwanda Paul Kagame na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, wamesema wanatarajia kuanza kutekelezwa kwa mpango tata wa kusafirishwa kwa wahamiaji kutoka London kwenda Kigali hivi karibuni.

Mpango huo umekuwa ukipingwa na wanaharakati wa haki za binadamu.
Mpango huo umekuwa ukipingwa na wanaharakati wa haki za binadamu. © AFP - Ben Stansall
Matangazo ya kibiashara

Hili limebainika baada ya ziara ya rais Kagame jijini London na kukutana na Sunak siku ya Jumanne, ambapo viongozi hao walijadiliana kuhusu mpango huo ambao umeendelea kupingwa na wanaharakati za haki za binadamu.

Tangu mwaka uliopita, Uingereza imekuwa ikitaka kuwasafirisha wahamiaji wanaowasili nchini humo kwa usafiri wa boti ndogo ndogo kwenda kupewa hifadhi nchini Rwanda, lakini mpango huo umekwama kwa sababu za kisheria.

Hata hivyo, kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mpango huo, wabunge nchini Uingereza wanapaswa kupitsiha sheria, itakayowezesha serikali ya nchi hiyo kuwahamishia nchini Rwanda wahamiaji haramu wanaoingia nchini humo.

Mswada huo wa sheria unaolenga kuhakikisha kuwa hakuna zuio lingine la Mahakama, umepangwa kujadiliwa tena Aprilli tarehe 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.