Pata taarifa kuu

Sudan Kusini : Zoezi la kuwaandikisha wapiga kura kuaanza mwezi Juni

Nairobi – Tume ya uchaguzi nchini Sudan Kusini, imetangaza kuwa, itaanza zoezi la kuwaandikisha wapiga kura mwezi Juni, kuelekea uchaguzi wa kwanza uliopangwa kufanyika nchini humo mwezi Desemba.

Salva Kiir- Rais wa Sudan Kusini.
Salva Kiir- Rais wa Sudan Kusini. AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume hiyo Abenego Akok amesema hatua hii inakuja baada ya kuchapishwa kwa ratiba ya uchaguzi huo wa kihistoria uliocheleweshwa kufanyika.

Licha ya kutangaza kuanza kwa zoezi la kuwaandikisha wapiga kura, Tume hiyo haijataja tarehe iliyotengewa kufanyika kwa uchaguzi huo, licha ya kukubaliwa kuwa ufanyike mwezi Desemba.

Hatua hii inakuja licha ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom, kuonya kuwa kwa mazingira yalivyo, ni vigumu kwa nchi hiyo kuandaa uchaguzi huru na haki.

Changamoto kubwa inayosalia ni utekelezwaji wa mkataba wa amani wa mwaka 2018 hasa kuundwa kwa jeshi moja kati ya kikosi cha rais Salva Kiir na Makamu wak Riek Machar, na kupatikana kwa katiba mpya.

Tangu ilipopata uhuru wake, ilipojitenga na Sudan, mwaka 2011 Sudan Kusini haijawahi kuandaa uchaguzi kutokana na mizozo na kisiasa na vita vya mara kwa mara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.