Pata taarifa kuu

Wananchi wa Burundi waadhimisha kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha rais Cyprien Ntaryamira

Wananchi wa Burundi waliadhimisha siku ya Jumamosi kumbukumbu ya miaka 30 tangu kuuawa kwa rais Cyprien Ntaryamira katika udunguaji wa ndege katika anga ya uwanja wa ndege wa Kanombe, iliyokuwa ikiwasafirisha na rais wa Rwanda Juvénal Habyarimana katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali. Tukio hilo lilitokea usiku wa Aprili 6 kuamkia Aprili 7, 1994.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye akiongozana na mkewe Angeline Ndayishimiye wakiongoza sherehe za Maadhimisho ya Miaka 30 ya kifo cha rais Cyprien Ntaryamira zilizofanyika Jumamosi Aprili 6, 2024 jijini Bujumbura.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye akiongozana na mkewe Angeline Ndayishimiye wakiongoza sherehe za Maadhimisho ya Miaka 30 ya kifo cha rais Cyprien Ntaryamira zilizofanyika Jumamosi Aprili 6, 2024 jijini Bujumbura. © Ntare Rushatsi House
Matangazo ya kibiashara

Rais Cyprien Ntaryamira ambaye aliongoza Burundi katika kipindi kigumu cha machafuko ya wenyewe kwa wenyewe, aliuawa April 6 mwaka 1994 jijini Kigali akiwa katika ndege iliyokuwa ikiwasafirisha yeye na mwenzike wa Rwanda Juvénal Habyarimana wakati ndege yao ikijaribu wakitua kwenye uwanja wa ndege wa Kanombe wakitokea jijini Arusha nchini Tanzania.

Cyprien Ntaryamira (Machi 6, 1955 - Aprili 7, 1994) alikuwa rais wa Burundi kutoka kabila la Wahutu walio wengi nchini humo, kutoka tarehe 5 Februari 1994 hadi kifo chake miezi miwili baadaye, wakati ndege aliyokuwa akisafiri, pamoja na rais wa Rwanda Juvénal Habyarimana, ilidnguliwa kwa bomu kwenye anga ya uwanja wa ndege wa Kanombe jijini Kigali, nchini Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.