Pata taarifa kuu

Rwanda kuaanza maadhimisho ya miaka 30 baada ya mauaji ya kimbari

Nairobi – Rwanda hapo kesho itaanza maadhimisho ya miaka 30 baada ya kutokea kwa mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 800,000 wengi wao Watutsi.

Madhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani ya nje ya bara la Afrika
Madhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani ya nje ya bara la Afrika © AFP / YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Madhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani ya nje ya bara la Afrika.

Kwa kipindi cha wiki moja, Wanyarwanda watatumia kipindi hicho cha kumbukukumbu ya kitaifa, kuwakumbuka jamaa, ndugu na marafiki waliopoteza maisha wakati wa mauaji hayo yaliyoduumu kwa zaidi ya siku 100.

Miaka 30 baadaye, Rwanda imekuwa imeendelea kujijenga upya chini ya uongozi wa rais Paul Kagame, ambaye ataongoza maadhimisho hayo kwa kuwasha mshuma wa kumkumbuku kwenye eneo la makumbusho linaloaminiwa kuwa watu zaidi ya 250,000 walizikwa kwa pamoja jijini Kigali.

Dunia imetakiwa kujifunza kutokana na kilichotokea nchini Rwanda kwa kuepuka chuki.
Dunia imetakiwa kujifunza kutokana na kilichotokea nchini Rwanda kwa kuepuka chuki. © Ben Curtis / AP

Kuanzia Jumapili, bendera zitapepea nusu mlingoti, na matamasha ya muziki, michezo na matukio mengine ya burudani hayatakubaliwa isipokuwa nyimbo za maombolezo zitakazochezwa kwenye Runinga na Redio za nchi hiyo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kupitia ujumbe wake wa vídeo utakaochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, amesema Ufaransa na washirika wake kutoka nchi za Magharibi na Afrika, walikuwa na uwezo wa kusitisha mauaji hayo, lakini hawakuwa na utashi huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guteress kwenye ujumbe wake amesema maadhimisho ya mwaka huu yanaikumbusha dunia, kutokubali kugawanyika tena kwa chuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.