Pata taarifa kuu

Uganda: UN yakosoa hatua ya mahakama kukataa kubatilisha sheria ya ushoga

Nairobi – Ofisi ya tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, imekosoa uamuzi wa mahakama ya kikatiba nchini Uganda, ambayo ilikataa kubatilisha sheria kali iliyopitishwa na bunge kuhusu ushoga.

Sheria hiyo ilipitishwa mwezi Mei mwaka jana, hatua ambayo ilikashifiwa vikali na watetezi wa masuala ya LGBTQ
Sheria hiyo ilipitishwa mwezi Mei mwaka jana, hatua ambayo ilikashifiwa vikali na watetezi wa masuala ya LGBTQ AP
Matangazo ya kibiashara

Watetezi wa haki za binadamu, walifungua shauri hilo kutaka mahakama iiagize Serikali kuondoa sheria hiyo, wanayosema kandamizi dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Tangu rais Yoweri Museveni, aidhinishe sheria hiyo, Uganda imekuwa ikinyooshewa kidole kwa kuwa na sheria gandamizi, huku mashirika kadhaa ya kimataifa yakitangaza kusitisha misaada kwa nchi hiyo. Stephane Dujarric, ni msemaji wa umoja wa Mataifa.

“Volker Turk ameeleza kusikikitishwa kwake na uamuzi wa mahakama ya kikatiba nchini Uganda kudumisha sheria ya kibaguzi ya kupinga ushoga.” alisema Stephane Dujarric, ni msemaji wa umoja wa Mataifa.

00:32

Stephane Dujarric, ni msemaji wa umoja wa Mataifa

Mahakama ya Katiba nchini Uganda wiki hii ilikataa ombi la kubatilisha sheria tata ya kupinga ushoga ambayo imeelezwa kuwa moja ya sheria yenye adhabu kali zaidi duniani.Sheria hiyo ilipitishwa mwezi Mei mwaka jana, hatua ambayo ilikashifiwa vikali na watetezi wa masuala ya LGBTQ, wanaharakati wa haki za binadamu, Umoja wa Mataifa na mataifa ya Magharibi.

Sheria ya kupinga ushoga ya 2023 inatoa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ambapo pia wahusika wanaweza kukabiliwa na  adhabau kifo.

Kampala imepinga shinikizo kutoka kwa mashirika ya haki, Umoja wa Mataifa na serikali za kigeni kuitaka kufuta sheria.
Kampala imepinga shinikizo kutoka kwa mashirika ya haki, Umoja wa Mataifa na serikali za kigeni kuitaka kufuta sheria. © AP

Serikali ya Rais Yoweri Museveni imekashifiwa kwa kutia saini sheria hiyo, mamlaka ikizishutumu nchi za Magharibi kwa kujaribu kuishinikiza Afrika kukubali ushoga.

Kwa mujibu wa waliokata rufa dhidi ya sheria hiyo, walisema kuwa inakiuka haki za kimsingi kwa mujibu wa katiba ya Uganda, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kutobaguliwa na haki ya faragha.

Mahakama ilikuwa imeanza kusikiliza kesi hiyo mwezi Disemba. Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja havikukabiliki nchini Uganda.

Bendera ya LGBTQ
Bendera ya LGBTQ AP - Lee Jin-man

Kampala imepinga shinikizo kutoka kwa mashirika ya haki, Umoja wa Mataifa na serikali za kigeni kuitaka kufuta sheria.

Benki ya Dunia ilitangaza mwezi Agosti kuwa inasitisha mikopo mipya kwa Uganda kutokana na sheria hiyo, ambayo kwa mujibu wake inakinzana na maadili yaliyowekwa na benki hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.