Pata taarifa kuu

Rwanda kuanza maadhimisho ya kitaifa ya miaka 30 kukumbuka mauaji ya kimbari

Nairobi – Rwanda kuanzia siku ya Jumapili, itaanza maadhimisho ya kitaifa ya miaka 30 kukumbuka mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya laki nane kwa kipindi cha siku 100 wengi wakiwa Watutsi.

Kumbukizi ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda inaanza rasmi tarehe 7 Aprili na itafikia kilele chake tarehe 13 mwezi huu.
Kumbukizi ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda inaanza rasmi tarehe 7 Aprili na itafikia kilele chake tarehe 13 mwezi huu. AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Kuelekea maadhimisho hayo, mwandishi wetu wa Kigali Christopher Karenzi amezungumza na baadhi ya manusura.

Katika kipindi hiki Wanyarwanda wanaomboleza familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza maisha yao kutokana na maujai ya kimbari yaliyofanyika mwaka 1994 nchini Rwanda.

Nshimiyimana Sam Gody ni mmoja wa walionusurika.

“Nilivonusurika sio rahisi kueleza wakati huo nilikuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Kiberinka nilikuwa nikiwindwa sana. Nilianza kutafuta sehemu za kujificha. Mauaji ya kimbari yalianza nikiwa nimejificha sehemu ya siri tena mbali kutokana na maandishi yangu ambayo hayakuwafurahisha.” alisema Nshimiyimana Sam Gody ni mmoja wa walionusurika.

00:24

Nshimiyimana Sam Gody ni mmoja wa walionusurika

Naye Gakuba Abadul Djabari ambaye alipoteza wazazi na wadogo zake wote, anaeleza hali ilivokuwa katika kipindi hicho kigumu na alivonusurika mauaji hayo

“Nilinusurika mmoja kutoka katika familia ya watu watano ambapo wengine wote wanne waliuawa.” alisimuliaGakuba Abadul Djabari.

00:15

Gakuba Abadul Djabari

Kumbukizi ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda inaanza rasmi tarehe 7 Aprili na itafikia kilele chake tarehe 13 mwezi huu ambapo bendera zitashushwa nusu mlingoti katika kipindi cha wiki nzima.

Christopher Karenzi Kigali, RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.