Pata taarifa kuu

Uganda: Mahakama ya katiba imekata ombi la kufuta sheria dhidi ya ushoga

Nairobi – Mahakama ya Katiba nchini Uganda imekataa ombi la kubatilisha sheria tata ya kupinga ushoga ambayo imeelezwa kuwa moja ya sheria yenye adhabu kali zaidi duniani.

Mahakama ilikuwa imeanza kusikiliza kesi hiyo mwezi Disemba. Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja havikukabiliki nchini Uganda.
Mahakama ilikuwa imeanza kusikiliza kesi hiyo mwezi Disemba. Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja havikukabiliki nchini Uganda. © AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Jaji Richard Buteera, naibu jaji mkuu wa Uganda na mkuu wa mahakama, katika uamuzi huo wa kihistoria, amesema kuwa mahakama inakataa kubatilisha sheria ya kupinga ushoga ya 2023 kwa ujumla wake, wala haitatoa amri dhidi ya utekelezaji wake.

Sheria hiyo ilipitishwa mwezi Mei mwaka jana, hatua ambayo ilikashifiwa vikali na watetezi wa masuala ya LGBTQ, wanaharakati wa haki za binadamu, Umoja wa Mataifa na mataifa ya Magharibi.

Sheria ya kupinga ushoga  ya 2023 inatoa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ambapo pia wahusika wanaweza kukabiliwa na  adhabau kifo.

Bendera ya LGBTQ
Bendera ya LGBTQ AP - Lee Jin-man

Serikali ya Rais Yoweri Museveni imekashifiwa kwa kutia saini sheria hiyo, mamlaka ikizishutumu nchi za Magharibi kwa kujaribu kuishinikiza Afrika kukubali ushoga.

Kwa mujibu wa waliokata rufa dhidi ya sheria hiyo, walisema kuwa inakiuka haki za kimsingi kwa mujibu wa katiba ya Uganda, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kutobaguliwa na haki ya faragha.

Mahakama ilikuwa imeanza kusikiliza kesi hiyo mwezi Disemba. Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja havikukabiliki nchini Uganda.

Rais Museveni alitia saini sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja
Rais Museveni alitia saini sheria inayopinga mapenzi ya jinsia moja © SERIKALI YA UGANDA

Kampala imepinga shinikizo kutoka kwa mashirika ya haki, Umoja wa Mataifa na serikali za kigeni kuitaka kufuta sheria.

Benki ya Dunia ilitangaza mwezi Agosti kuwa inasitisha mikopo mipya kwa Uganda kutokana na sheria hiyo, ambayo kwa mujibu wake inakinzana na maadili yaliyowekwa na benki hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.