Pata taarifa kuu

Rwanda: HRW yataka kusakwa zaidi kwa watuhumiwa wa mauaji ya kimbari

Nairobi – Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, sasa linataka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya kuwasaka watuhumiwa zaidi wa mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda, ambapo mwishoni mwa juma hili, Kigali itafanya kumbukizi ya miaka 30.

Mwishoni mwa juma hili, Kigali itafanya kumbukizi ya miaka 30.
Mwishoni mwa juma hili, Kigali itafanya kumbukizi ya miaka 30. © SIMON WOHLFAHRT/AFP
Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch imetoa kauli hii, siku tano kabla ya kuanza kwa maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji hayo, yaliyosababisha vifo vya watu laki nane, wengi wao Watutsi kwa siku 100.

Shirika hilo limesema licha ya washukiwa wakuu wakiwemo, waliokuwa wakuu wa vitengo mbalimbali serikali kukamatwa na kufunguliwa mashtaka, kuna baadhi yao ambao bado hawajapatikana.

Aidha, katika ripoti yake, Shirika hilo linasema, baadhi ya washukiwa wamefariki dunia, huku wengine wakishindwa kufunguliwa mashtaka kwa sababu ya hali yao mbaya ya kiafya na umri wao mkubwa, lakini ikasisitiza kuwa ni lazima haki itendeke.

Mwezi Novemba mwaka uliopita, viongozi wa kimataifa wa mashtaka walibaini kuwa, mmoja wa washukiwa aliyekuwa anatafutwa Aloys Ndimbati, aliyekuwa amefariki dunia akiwa nchini Rwanda mwaka 1997.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa washukiwa wawili wakuu bado wanatafutwa ili kufunguliwa mashtaka, miaka 30 baada ya mauaji hayo mabaya katika historia ya Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.