Pata taarifa kuu

Kenya: Madaktari wanaogoma wakataa pendekezo la serikali la nyongeza ya mshahara

Nairobi – Chama cha Madaktari nchini Kenya, kinasema kimekataa kiwango cha pendekezo la nyongeza ya mshahara kilichopendekezwa na serikali wakati huu wanachama wake wakiendelea na mgomo kwa wiki ya tatu.

Madaktari wamekataa pendekezo la serikali kuhusu nyongeza ya mishahara.
Madaktari wamekataa pendekezo la serikali kuhusu nyongeza ya mishahara. REUTERS - Monicah Mwangi
Matangazo ya kibiashara

Hili limethibitishwa na Mwenyekiti wa chama hicho Abidan Mwachi, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.

Mwachi, amesema madai kuwa serikali imewalipa mshahara sio sahihi na wanaendelea na mgomo wao, ulioanza Machi 15 kudai malipo yao na kishinikiza kuajiriwa kwa Madaktari wanafunzi miongoni mwa madai mengine.

Siku ya Jumanne, serikali ilitoa wito kwa Madaktari hao kusitisha mgomo na kuahidi kutumia Dola Milioni 18.39 kuwaajiri Madaktari wanafunzi wiki hii.

Mvutano huu kati ya Madaktari na serikali umeendelea kuathiri huduma za afya kwenye hospitali za umma, ambapo wagonjwa wameendelea kuteseka na kushindwa kupata huduma muhimu.

Katika hatua nyingine, Mahakama ya kazi jijini Nairobi imetoa siku 14 kwa Madaktari na serikali kupata suluhu ya mvutano unaoshuhudiwa.

Serikali na Madaktari wamekuwa wakijadiliana tangu kuanza kwa mgomo huo bila mafanikio na uamuzi wa Mahakama unamaanisha kuwa huenda mgomo huo ukaendelea kwa wiki mbili zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.