Pata taarifa kuu

Watu 10 wamefariki katika ajali ya barabarani nchini Kenya

Nairobi – Watu 10 wamepoteza maisha nchini Kenya, kutoakana na ajali ya barabarani iliyohusisha magari matano, usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa polisi wa usalama barabarani, ajali nchini Kenya hutokea mara kwa mara kwa sababu ya uendeshaji wa kasi wa magari, madereva walevi lakini pia hali mbaya ya barabara
Kwa mujibu wa polisi wa usalama barabarani, ajali nchini Kenya hutokea mara kwa mara kwa sababu ya uendeshaji wa kasi wa magari, madereva walevi lakini pia hali mbaya ya barabara Google map
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo imetokea katika eneo linalofahamiaka kama Salama, katika barabara kuu ya kutoka jiji kuu la Nairobi, kwenda kwenye jii la Pwani Mombasa.

Kamanda wa Polisi kwenye hilo Barnabas Ng'eno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha basi ndogo lenye abairia 18 na lingine lenye abiria 14 yaliyogongana na magari mengine mawili.

Mbali na ajali hii, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chavakali amepoteza maisha katika ajali nyingine ya barabarani Magharibi mwa nchi hiyo, wakati basi lililokuwa linawasafirisha wanafunzi waliokuwa wanaelekea jijini Nairobi kwa ajili ya likizo fupi, kuanguka na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30.

Tangu mwezi Januari, zaidi ya watu Elfu moja wamepoteza maisha kutokana nan a ajali za barabarani nchini Kenya kwa mujibu wa Mamlaka ya usalama barabarani NTSA.

Kwa mujibu wa polisi wa usalama barabarani, ajali nchini Kenya hutokea mara kwa mara kwa sababu ya uendeshaji wa kasi wa magari, madereva walevi lakini pia hali mbaya ya barabara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.