Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Sudan Kusini: Wengi kutokuwa na uhakika na uchaguzi wa Desemba

Raia wenfgi wa Sudan Kusini hawana tena matumaini ya kufanyika kwa uchaguzi mwezi wa Desemba nchini humo. Kwa upande wa waangalizi, washirika wa kimataifa na mashirika ya kiraia nchini Sudan Kusini, wanaona kuwa mwezi wa Aprili unawakilisha fursa ya mwisho ya kuona uchaguzi wa kwanza katika historia ya nchi hiyo ukifanyika, kama ilivyopangwa, mwezi Desemba.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, na Makamu rais Riek Machar baada ya mkutano wao na waandishi wa habari mjini Juba, Desemba 17, 2019.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, na Makamu rais Riek Machar baada ya mkutano wao na waandishi wa habari mjini Juba, Desemba 17, 2019. Majak Kuany / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo changa zaidi duniani imekuwa ikisubiri kuwachagua wawakilishi wake tangu ilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Sudan mwaka 2011.

Baada ya vita mbaya vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mahasimi wawili Salva Kiir na Riek Machar kati ya mwaka 2013 na 2018, makubaliano ya amani yalianzisha serikali ya umoja wa kitaifa, na Bw. Kiir rais na Bw Machar makamu wa kwanza wa rais, wakati wa kipindi cha "mpito" kitakachomalizika kwa Uchaguzi Mkuu.

Lakini nchi imeendelea kuzoroteshwa na vita vya kuwania madaraka na mwisho wa kipindi cha "mpito" umeahirishwa mara kwa mara. Kulingana na makubaliano ya hivi punde Uchaguzi Mkuu umepangwa kufanyika mwezi Desemba 2024.

Je, hali ikoje?

"Nchi bado haiwezi kuandaa uchaguzi wa kuaminika," alionya mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Nicholas Haysom, mwezi Desemba 2023, akisisitiza kwamba idadi fulani ya "masharti muhimu" inapaswa kutimizwa kuwezesha uchaguzi wa amani mwezi Desemba. Miezi mitatu baadaye, hakuna maendeleo makubwa ambayo yameonekana.

"Muungano" wa vikosi vya usalama, ambayo ni kusema, ushirikiano wa vikosi vinavyomuunga mkono Kiir na Machar ndani ya jeshi moja na polisi, bado haujakamilika. Iwapo wanajshi na maafisa wa polisi 55,000 walipata mafunzo katika awamu ya kwanza, ni 4,000 pekee walitumwa, alibainisha mwezi wa Februari Meja Charles Tai Gituai, mkuu wa RJMEC, chombo kinachosimamia utekelezaji wa makubaliano ya amani. Na awamu ya pili inasalia "kutokuwa na uhakika".

Kutokuwepo kwa vikosi vya kijeshi vya kitaifa ni hatari sana katika nchi hii iliyoathiriwa na ghasia za kikabila (vifo 406 katika robo ya mwisho ya mwaka 2023, kulingana na Umoja wa Mataifa). Kwa kuzingatia uchaguzi huo, Baraza la Vyama vya Siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ziliundwa. Lakini hazifanyi kazi, kwa sababu ya ukosefu wa fedha, na zinakabiliwa na utata.

Uundwaji wao unakosolewa kuwa unaipendelea serikali na vyama vingi vya upinzani vinashutumu malipo "makubwa" ya usajili wa dola 50,000. Uandishi wa katiba, "ambao umechelewa kwa miezi 15" umepata maendeleo kidogokulingana na Nicholas Haysom Desemba mwaka, jana.

Uchaguzi unaowezekana mnamo Desemba?

Washirika wa kimataifa - ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, "troika" ambayo ilifadhili uhuru (Marekani, Uingereza, Norway) - wanaendelea kutoa wito kwa Salva Kiir na Riek Machar kufanya kazi kwa ajili ya uchaguzi. Rais, ambaye alifanya kazi ya kujumuisha mamlaka yake katika miezi ya hivi karibuni, amesisitiza nia yake ya kufikia makataa. Mpinzani wake alitangaza kwamba angesusia kura yoyote mradi tu vifungu muhimu vya makubaliano ya amani (ikiwa ni pamoja na kuandaa katiba ambayo itachukua, kulingana na yeye, miezi 24) haifanyi kazi.

"Salva Kiir ana nia ya uchaguzi (...) kwa sababu amechoshwa na mikono yake kufungwa na makubaliano ya amani" ambayo yanasambaza madaraka, anakadiria Boboya James Edimond, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Sera na Utafiti wa Jamii (ISPR), kituo cha fikra kilichopo Juba. "Riek Machar anaogopa kupoteza mamlaka," anaendelea: "Nia yake kwa hiyo ni kuhakikisha kwamba vipengele vyote vya mkataba wa amani vinatekelezwa (...) ili kukaa madarakani kwa muda mrefu iwezekanavyo ".

Kuandaa uchaguzi katika kipindi cha miezi minane kunaonekana kuwa ngumu katika nchi yenye miundombinu duni, inayokumbwa na ukosefu wa usalama na kunyimwa mapato muhimu ya mafuta kutokana na kuzimwa kwa bomba la mafuta lililoharibiwa nchini Sudan inayokumbwa na vita. "Iwapo tungeharakisha uchaguzi, kuna uwezekano mkubwa kwamba nchi inaweza kurejea tena kwenye vurugu," anaonya Edmund Yakani, kiongozi wa shirika la kiraia: "Ni muhimu kuwa na maelewano sio kuwaharakisha, lakini pia ili tusiwacheleweshe sana."

Uchaguzi "uliopunguzwa" au upanuzi wa kipindi cha mpito?

Katika barua ya Machi 15, RJMEC ilitoa wito kwa wahusika kujadili "chaguzi zinazowezekana": "kufanya uchaguzi uliopunguzwa" au "kurekebisha makataa ya 'yaliyopendekezwa'". Chama cha rais kilipendekeza "uchaguzi mkuu" mwezi wa Desemba kuteua rais na magavana wa majimbo, kisha uchaguzi wa wabunge mwaka mmoja baadaye. Riek Machar alijibu kuwa yuko tayari kwa "mazungumzo" na mpatanishi.

Kwa mujibu wa Edmund Yakani, mazungumzo kama hayo yasiishie tu kwa watendaji wa kisiasa, wakiongozwa na masilahi yao, bali pia mashirika ya kiraia (viongozi wa kidini, vijana, wanawake, nk). "Wananchi hawataki kuongezewa muda (wa mpito) kwa sababu umenyonywa kwa miaka mitano iliyopita bila maendeleo yoyote," anaonya. Ikiwa viongozi wataahirisha tena uchaguzi, "tunahitaji ratiba iliyo wazi", anabainisha, akisisitiza uharaka wa hali hiyo: "Ikiwa hakuna uamuzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.