Pata taarifa kuu

RDC: Olive Lembe, Mke wa rais mstaafu Joseph kabila amezuru Goma

Nairobi – Mke wa rais mstaafu wa DRC Olive Lembe, hapo jana alifanya ziara kwenye mji wa Goma kwa kutembelea kambi kadhaa za wakimbizi, ambapo amelaani machafuko yanayoendelea mkoani Kivu Kaskazini, akiwalaumu viongozi wa sasa kwa kushindwa kuleta utulivu kwenye eneo la mashariki.

Olive Lembe amelaani machafuko yanayoendelea mkoani Kivu Kaskazini, akiwalaumu viongozi wa sasa kwa kushindwa kuleta utulivu kwenye eneo la mashariki.
Olive Lembe amelaani machafuko yanayoendelea mkoani Kivu Kaskazini, akiwalaumu viongozi wa sasa kwa kushindwa kuleta utulivu kwenye eneo la mashariki. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Akiwahotubia maelfu ya raia waliokimbia vita na ambao kwa sasa wanaishi katika kambi za wakimbizi nje kidogo na mji wa Goma, Olive Lembe mkewe rais mtstaafu wa DR Congo Joseph kabila amesema:

“Mwenyezi Mungu anaweza kutusaidia kupitia wino aliyoweka kwenye kalamu yake Joseph Kabila ili matatizo tunayokumbana nayo kwa sasa yafike mwisho.” Alisema Olive Lembe.

00:11

Olive Lembe mkewe raisi mtstaafu wa DR Congo Joseph kabila

Akilitumia kwa mara kadhaa jina la Mungu, Lembe mwenye ushawishi mkubwa katika siasa nchini DRC, amedai kuwa Joseph alilisaidia taifa hilo kupata amani baada ya miongo kadhaa za machafuko.

“Alileta ahdai za kuinganisha nchi yetu na ikwawa hivyo, kila mtu alikuwa na uhuru wakuzunguka sehemu zote bila tatizo,na hilo likatimiza ahadi zote alizo tutolea.”AliongezaOlive Lembe.

00:12

Olive Lembe kuhusu ahadi za Joseph Kabila

Siraji Nyalamba ni afisa mkuu wa chama tawala, UDPS mkoani kivu kaskazini.

“Na hitaji kufahamu ni aina gani ya amani anayo zungumzia kuhusu Kabila .Uongozi wao uligubikwa na umwagaji wa damu. Kwa muhula wote wake kulishuhudiwa ongezeko la makundi ya waasi.”alielezaSiraji Nyalamba.

00:10

Siraji Nyalamba ni afisa mkuu wa chama tawala, UDPS mkoani kivu kaskazini

Hayo yanajiri siku chache tu baada yake katibu mkuu wa chama cha tawala Udps Augustin Kabuya kutangaza kuondoka kwa siri hapa nchini DRC kwa rais huyo mstaafu.

Tuhuma hizo zilitupiliwa mbali na uongozi wa kambi yake Joseph Kabila. 

Benjamin Kasembe- Goma RFI Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.