Pata taarifa kuu

Rais Kagame amesema nchi yake haiwezi kuzidi kulaumiwa kwa matatizo ya DRC

Nairobi – Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kwa mara nyingine amerejelea kauli yake kuwa, Kigali haiwezi kuendelea kulaumiwa kwa matatizo yanayoshuhudiwa DRC na hasa hali ya usalama mashariki mwa nchi hiyo.

 Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Kagame amesema haya katika mahojiano na vituo kadhaa vya habari vya ndani jijini Kigali.

Katika mahojiano Maalum na vituo vya Radio10 na Royal FM, Kagame amesema Rwanda kwa muda mrefu imekuwa ikilaumiwa kwa matatizo ya jirani yake, na kaongeza kuwa wakati sasa umefika kwa watu wa Congo kutathmini maswala yao ya kiutawala.

Tatizo la mashariki mwa Congo linatokana na Congo na uongozi wake, alisema rais Kagame, wakati mwingine, watu huweka mzigo wa Kongo kwenye mabega ya Rwanda, Mzigo wa DRC lazima uchukuliwe na watu wa Kongo na viongozi wao na sio Wanyarwanda au viongozi wa Rwanda.

Kigali na Kinshasa zimekuwa zikituhumiana kuhusu utovu wa usalama mashariki ya DRC.
Kigali na Kinshasa zimekuwa zikituhumiana kuhusu utovu wa usalama mashariki ya DRC. © Jorge Nsimba AFP montage RFI

Rais Kagame amesema Rwanda yenyewe ina matatizo yake ambayo kwa ushirikiano wa pamoja na wananchi wanajaribu kuyatatua, matamshi anayoyatoa siku chache kupita tangu afanye mahojaino mengine na kuwakosoa viongozi wa Congo kwa kile alisema kuficha madhaifu yao kwa mgongo wa Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.