Pata taarifa kuu

Tanzania: Mashirika ya Kenya yatiwa wasiwasi kuhusu utoaji wa vibali vipya vya kuwinda tembo

Wasiwasi unaendelea nchini Kenya kwa "Super Tuskers", ndovu hawa wakubwa wenye meno marefu sana ambayo yanaweza kuwa na uzito wa hadi kilo 45. Wanyama watatu kati ya hawa wakubwa wameuawa katika muda wa miezi sita iliyopita kwenye mpaka na Kenya. Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayolinda wanyamapori yana wasiwasi hasa kwa sababu vibali vitatu vipya vya uwindaji vimetolewa, wakati zinasalia ndovu wakubwa "super Tuskers" wisiyozidi 50 barani Afrika.

Tembo wa Kiafrika anaweza kutoweka kwa muda mfupi, mwathirika wa ujangili wa pembe za ndovu, wataalam wanaonya. (Picha ya kielelezo)
Tembo wa Kiafrika anaweza kutoweka kwa muda mfupi, mwathirika wa ujangili wa pembe za ndovu, wataalam wanaonya. (Picha ya kielelezo) AFP/Roberto SCHMIDT
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu katika eneo hilo, Albane Thirouard

Uwindaji umeidhinishwa nchini Tanzania lakini tangu miaka 30 iliyopita, wanyama wenye umbo kubwa wamekuwa wakilindwa kwa makubaliano. Kulingana na mkataba huo, "Super Tusker", tembo hao wa Kiafrika ambao meno yao yanaweza kuwa na uzito wa kilo 45, wanalindwa katika eneo la mpaka kati ya Kenya na Tanzania.

Lakini katika miezi ya hivi karibuni, tembo watatu wakubwa wameuawa kwa upande wa Tanzania. Je, mkataba huu sasa umepitwa na wakati? Hivi ndivyo gavana wa Kaunti ya Kajiado, nchini Kenya, anajutia, ambapo wanyama ni rasilimali kuu kwa utalii. Hapa, Hifadhi ya Kitaifa ya Amboseli inapakana na Tanzania. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, anaonyesha "wasiwasi wake wa kina" na vibali vipya vya uwindaji vilivyotolewa "huongeza tu wasiwasi kuhusu siku zijazo za viumbe hawa wa kitabia", anakosoa.

Mashirika ya ulinzi wa wanyamapori pia yana wasiwasi. "Uwindaji huu kwa hakika ni halali nchini Tanzania lakini si jambo sahihi," anashutumu Cynthia Moss, mwanzilishi wa hazina ya tembo ya Amboseli. “Wawindaji huwalenga hasa tembo dume wenye umri mkubwa. Hao ndio wenye ulinzi mkubwa lakini kwa bahati mbaya, ndio ambao wako kwenye kilele cha kazi yao ya uzazi. Na hii, wakati kukiwa na takriban Super Tuskers kumi pekee waliosalia katika eneo la mpaka wa Kenya na Tanzania,” analaumu.

Kwa hivyo gavana wa Kajiado anatoa wito kwa mamlaka za Tanzania kuzingatia matokeo ya maamuzi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.