Pata taarifa kuu

RDC: Wakimbizi washindwa kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka

Nairobi – Wakati Wakiristo duniani wanapojiandaa kuadhimisha sikukuu ya Pasaka hapo kesho, maelfu ya wakimbizi wakristo waishio katika kambi mbalimbali nje kidogo ya mji wa Goma, wanasema hali ngumu ya maisha imewafanya kushindwa kujiandaa kwa ajili ya sikukuu hiyo.

Wakaazi wa DRC wanaoishi katika kambi za wakimbizi wameeleza changamoto wanazokabiliwa nazo wakati huu wa Pasaka.
Wakaazi wa DRC wanaoishi katika kambi za wakimbizi wameeleza changamoto wanazokabiliwa nazo wakati huu wa Pasaka. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

Lushagala ni moja kati ya kambi zinazo hifadhi idadi kubwa ya watu waliokimbia mapigano baina ya jeshi la serikali na waasi wa M23, Lakini hii juma pili hakuna dalili za maadhimisho ya pasaka .Baadhi ya wakimbizi hao wamekosa chakula na bidhaa zingine muhimu.

"Hatuna uwezo wakuandaa pasaka kwa sababu hatuna chochote na hata tunasumbuliwa na msongo wa mawazo." alisema mmoja wa wakimbizi.

Kama ilivyo kote duniani,pasaka ni sikukuu muhimu  kwa Wakristo nchini DRC lakini mwaka huu imekuwa ni tofauti.Sofia Agnes ni mama anayeishi ndani ya kambi ya lushagala.

 "Tunatoa wito kwa viongozi wetu wa nchi watusaidie ili tuadhimishe sikukuu hii ya pasaka ambayo ni siku kuu muhimu iliyotukomboa." alieleza Sofia Agnes ni mama anayeishi ndani ya kambi ya lushagala.

Wakristo wengi katika kambi za wakimbizi wamekuwa wakihisi kuwa wametelekezwa tangu kuzuka upya kwa vita hivyo vinavyo tatiza maadhimisho ya sherehe mbalimbali ikiwemo pasaka.

Ripoti ya umoja wa mataifa imesema kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani imefikia zaidi ya milioni 6 kutokana na kusambaa kwa vita  mkoani kivu kaskazini.

Benjamin Kasembe- RFI Kiswahili, Goma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.