Pata taarifa kuu

Msafara wa wanajeshi wa UN washambuliwa mjini Butembo DRC

Nairobi – Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na gari la Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC kuchomwa moto wakati wa makabiliano kati ya vijana na walinda amani katika eneo la Mutshanga, kaskazini mwa mji wa Butembo mapema leo ijumaa. Maafisa wa usalama wanasema msafara wa jeshi la walinda amani ulikuwa ukitokea Rwindi kuelekea mji wa Beni kaskazini zaidi mwa mkoa wa Kivu kaskazini.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakisaidia katika juhudi za kurejesha utulivu Mashariki ya DRC.
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakisaidia katika juhudi za kurejesha utulivu Mashariki ya DRC. © MONUSCO
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na vyombo vya habari katika mji huo wa Butembo, Edgard Mateso mkaazi wa eneo hilo amefahamisha kuwa vijana walishambulia gari la MONUSCO ambalo lilipotea kutoka kwenye barabara inayounganisha miji ya Butembo na Beni baada ya kubaki nyuma kwenye msafara huo.

Kupotea kwa gari hilo kulisababisha hofu miongoni mwa raia kwa sababu watu hawakuelewa ni kwa namna gani gari linalopaswa kwenda Beni lipatikane katika eneo tofauti, upande wa mashariki.

Mateso anasema dereva alijikuta amezungukwa na vijana kadhaa, na kwamba alitaka kurudi kwa bahati mbaya gari lake lilitumbukia kwenye mtaro, na kwamba isingalikuwa msaada kutoka kwa jeshi la serikali FARDC ambao waliingilia kwa kufyatua risasi juu kuwatawanya vijana hao, basi huenda hata dereva angeuawa.  

MONUSCO imeanza kuondoka nchini DRC baada ya utawala wa Kinshasa kuwataka kuondoka.
MONUSCO imeanza kuondoka nchini DRC baada ya utawala wa Kinshasa kuwataka kuondoka. © Photo MONUSCO/Force

Kwa upande wake mwenyekiti wa mashirika ya kiraia kwenye mji wa Butembo, Mathe Saanane amefahamisha kuwa mwathiriwa aligongwa na risasi  alipokuwa kwenye shughuli zake karibu na eneo la tukio.

Tukio la pili lilitokea umbali wa kilomita 10, karibu na kijiji kinachofahamika kama Amini Yesu, kwenye barabara ya Beni-Butembo, ambapo vyanzo vya kijeshi vya MONUSCO vimesema vifaa vyao vilishambuliwa na kurushiwa mawe kutoka kwa waandamanaji waishio wilayani Furu, ambapo lori lingine pia lilichomwa moto.

Taarifa zaidi zinasema msafara ulioshambuliwa ulikuwa ukirejea kutoka Rwindi katika eneo la Rutshuru kuelekea mji wa Beni, kama sehemu ya kuondolewa kwa MONUSCO katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.