Pata taarifa kuu

Mwenyekiti wa EAC aendelea na ziara yake katika nchi za Ukanda

Nairobi – Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, hapo jana amezuru nchi ya  Angola katika mfululizo wa ziara zake kwenye nchi za Ukanda, akitokea nchini DRC, ambako alikutana na rais Felix Tshisekedi, na kuzungumza kuhusu hali ya usalama mashariki mwa Congo.

Rais Kiir pia amezuru nchi za Rwanda na Burundi.
Rais Kiir pia amezuru nchi za Rwanda na Burundi. © RDC Statehouse
Matangazo ya kibiashara

Akiwa Kinshasa, rais Kiir, mbali na kutaka kupatikana haraka kwa suluhu ya changamoto ya usalama mashariki mwa DRC na kwenye ukanda, pia alitoa wito wa kufufuliwa kwa mpango wa amani wa Nairobi na Luanda.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na viongozi hao, Kiir alitaka michakato yote miwili kuheshimiwa ili kuhakikisha inatoa suluhu ya kudumu kwa mzozo unaoendelea mashariki mwa DRC.

Kutoka Kinshasa, rais Kiir sasa yuko mjini Luanda, ambako anakutana na rais Joao Laurencio, anayeratibu mazungumzo kati ya rais Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, lengo likiwa kuzungumzia hatua zilizofikia.

Kabla ya kufika Kinshasa, rais Kiir alizuru nchini ya Rwanda na kukutana na rais Kagame, kabla ya kuelekea Rwanda ambako alikutana na rais Evariste Ndayishimiye, ikiwa ni katika juhudi za kusaidia kupata suluhu ya mgogoro unaoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.