Pata taarifa kuu

Rwanda: Denis Kazungu amehukumiwa maisha jela kwa makosa ya mauaji

Nairobi – Raia wa Rwanda Denis Kazungu amehukumiwa maisha jela na Mahakama jijini Kigali baada ya kupatikana na kosa la mauaji ya watu kadhaa, ambao miili yao ilipatikana imezikwa nyumbani kwake mwaka uliopita.

Ramani ya Rwanda ikionesha nchi hiyo ilivyo
Ramani ya Rwanda ikionesha nchi hiyo ilivyo © fmm
Matangazo ya kibiashara

Kazungu alikamatwa mwezi Septemba mwaka uliopita, baada ya polisi kufanya msako nyumbani kwake jijini Kigali na kugundua miili ya watu hao.

Alikiri kuwauwa watu 14, akiwemo mwanaume, akidai walimuambukizwa virusi vya Ukimwi.

Wakati kesi yake ikisilikizwa aliomba msamaha na kuiomba Mahakama isimpe adhabu kali.

Wakati wa hukumu hiyo iliyotolewa jana, Kazungu mwenye umri wa miaka 34 hakuwepo Mahakama, wakati Jaji wa Mahakama Kuu alipompata na makosa ya mauji, ubakaji na kuhifadhi miili ya watu.

Haijafahamika iwapo Kazungu ambaye aliwahi kuwa Mwalimu wa Kiingereza atakata rufaa baada ya kupewa adhabu, baada ya siku 30 kwa mujibu wa sheria za Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.