Pata taarifa kuu

Uganda : Serikali kupitia upya sera yake ya kuwapa hifadhi wakimbizi

Nairobi – Serikali ya Uganda, inasema huenda ikalazimika kupitia upya sera yake ya kuwapa hifadhi wakimbizi, ikiwa jumuiya ya kimataifa itaendelea kusalia kimya katika kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na ongezeko la wakimbizi.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. AP - Bebeto Matthews
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri wa misaada na kukabiliana na majanga, Hilary Onek, amesema nchi yake inahangaika kupta kiasi cha dola za Marekani milioni 800 na bilioni 1 zinazohitajika kwa mwaka ili kuwahudumia wakimbizi.

Onek, anasema ikiwa hali itaendelea kuwa mbaya na kama hawatapata fedha hizo kwa wakati, basi hawatakuwa na lakufanya zaidi ya kupitia upya sera yake kuhusu wakimbizi.

Waziri huyo ameongeza kuwa sera yake ya sasa inawagharimu, na kwamba wakati umefika kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati kuisaidia ili iweze kuhudumia idade kubwa ya wakimbizi wanaoendelea kuwasili nchini humo.

Kwa sasa nchi ya Uganda, inatoa hifadhi kwa wakiùbizi zaidi ya milioni 1 na laki 6.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.