Pata taarifa kuu

DRC: Wakuu wa majeshi ya SADC wamekutana na wenzao wa FARDC

Nairobi – Wakuu wa majeshi kutoka nchi za SADC zilizochangia katika kikosi cha pamoja SamiDRC, wamekuwa na mkutano na viongozi wa jeshi la Congo, FARDC mjini Goma, kujadiliana namna ya kutekeleza operesheni dhidi ya makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo.

Wanajeshi kutoka nchi za SADC walitumwa nchini DRC kusaidia katika urejeshaji wa usalama mashariki ya nchi.
Wanajeshi kutoka nchi za SADC walitumwa nchini DRC kusaidia katika urejeshaji wa usalama mashariki ya nchi. REUTERS - ARLETTE BASHIZI
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao kutoka nchi za Tanzania, Afrika Kusini, Burundi na Malawi, watafanya ziara katika maeneo kadhaa ya mashariki mwa Congo, kutathmini na kuweka mikakati ya kukabiliana na waasi wa M23 wanaojaribu kusogelea mji wa Goma.

Mkutano huu umekuja baada ya mikutano mingine iliyofanyika majuma kadhaa yaliyopita, ambapo wakuu wa nchi hizo kando na kuhudhuria shughuli za mazishi ya rais wa zamani wa Namibia, juma lililopita, walikutana na rais Felix Tshisekedi.

Licha ya kuwa tayari mataifa hayo yametuma wanajeshi Wake mashariki mwa nchi hiyo, bado hawajaanza kutekeleza operesheni rasmi za kijeshi dhidi ya waasi hao wanaodaiwa kusaidiwa na serikali ya Rwanda.

Vikosi vya SamiDRC, vinachukua majukumu ya vile vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki vilivyoondoka mwishoni mwa mwaka jana kufuatia maagizo ya utawala wa Kinshasa, sambamba na vile vya umoja wa Mataifa MONUSCO ambavyo na vyenyewe vimeanza kuondoka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.