Wanajeshi wa Afrika Kusini wauuawa mashariki mwa DRC
Nairobi – Wanajeshi wawili wa Afrika Kusini wameuawa wakati wengine watatu wakiripotiwa kujeruhiwa katika shambulio kwenye moja ya kambi zao za kijeshi nchini DRC ambapo walitumwa kukabiliana na makundi ya waasi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Maofisa hao wamekuwa waathiriwa wa kwanza tangu Afrika Kusini kuanza kuwatuma maofisa wake wa jeshi nchini DR Congo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka uliopita.
Shambulio hilo limetokea katika mji wa Sake, karibia kilomita 27 Magharibi mwa mji wa Goma.
Kwa mujibu wa taarifa iliochapishwa kwenye ukurasa wa X, jeshi la Afrika Kusini limesema uchunguzi umeanza kuhusiana na tukio hilo.
The SA National DefenceForce Media Statement || Thursday, 15 February 2024 || The SA National DefenceForce soldiers deployed in the SADC Mission in the Democratic Republic of the Congo were injured during an indirect fire.#SANDF#JointOperationsDivision#RIPSASoldiers#DRC pic.twitter.com/cIoxX2E5sw
— SA National Defence Force (@SANDF_ZA) February 15, 2024
Wanajeshi wa Afrika Kusini pamoja na wanajeshi kutoka Tanzania na Malawi ni sehemu ya ujumbe wa Kusini mwa Afrika ulio nchini DR Congo (SAMIDRC), ambao ulitumwa kusaidia serikali kuleta amani, usalama na utulivu mashariki mwa nchi hiyo kunakokabiliwa machafuko.
Jumatatu iliyopita, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa aliamuru kutumwa kwa wanajeshi 2,900 nchini DRC.
Mapigano ya hivi majuzi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha makumi ya maelfu ya watu kuyahama makazi yao.