Pata taarifa kuu

DRC: Waziri Jean Pierre Bemba amefanya ziara mjini Goma

Nairobi – Waziri wa ulinzi nchini DRC, Jean Pierre Bemba, aliwasili jijini GOMA hapo jana, ziara yake anayoifanya wakati huu vikosi vya serikali vikizidisha mashambulio dhidi ya waasi wa M23 waliokuwa wanadaiwa kuelekea kwenye mji huo.

Waziri wa ulinzi nchini DRC, Jean Pierre Bemba
Waziri wa ulinzi nchini DRC, Jean Pierre Bemba REUTERS/Jerry Lampen
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri Bemba, alikuwa Goma kuwaona waliojeruhiwa kutokana na vita pamoja na kuzisaidia familia 12 zilizowapoteza wapendwa wao kuweza kuwazika waliofariki.

“Ni ujumbe wa faraja na kutoa msaada pia kwa rafiki zetu wanajeshi waliopo hapa wa SADC, makampuni binafsi ndugu zetu wazalendo,ambao nao wanapigana tunawapongeza kwa ulinzi wa eneo letu " alisema waziri Bemba.

00:17

Waziri wa ulinzi nchini DRC, Jean Pierre Bemba

Aidha kiongozi huyo alitoa wito kwa raia katika mkoa wa Kivu kaskazini kuwa watulivu wakati huu ambapo mkuu wa nchi anafuatilia kwa karibu hali kwenye eneo hilo.

Vilevile amewaeleza raia kuwa jeshi la nchi yake linafanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa Goma, Sake na maeneo mengine yote yanalindwa pamoja na eneo lote na Masisi na Rutshuru ilikuona kuwa raia wanakombolewa kutoka kwa M23.

Pasi Mubalama anatoka katika shirika la kiraia la wanawake la Aidprofen.

“Ni sharti wapigane iliwawaondoe M23 kila mahali ambapo wanapopatikana kwa sababu sio Goma tu.” alieleza Pasi Mubalama.

00:11

Pasi Mubalama

Haya yanajiri wakati pia Ufaransa ikilaani kuendelea kwa mashambulio ya M23 pamoja na mashambulio yoyote dhidi ya kikosi cha MONUSCO.

CHUBE NGOROMBI GOMA RFI kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.