Pata taarifa kuu

DRC: Mapigano makali kati ya M23 na jeshi la serikali yaripotiwa

Nairobi – Mapigano makali kati ya waasi wa M 23 na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jimboni Kivu Kaskazini yamesababisha vifo vya maafisa 17 wa jeshi na wapiganaji wa wazalendo wanaowaunga mkono.

Vita hivyo vimeendelea kusababisha wasiwasi, na hata kusababisha wakaazi wa Sake kuanza kuyakimbia makaazi yao
Vita hivyo vimeendelea kusababisha wasiwasi, na hata kusababisha wakaazi wa Sake kuanza kuyakimbia makaazi yao © ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Habari la Ufaransa AFP limesema limepata taarifa hizo za mauaji kutoka kwa maafisa wa usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wiki hii kumeshuhudiwa mapigano makali kati ya waasi wa M 23 dhidi ya jeshi la serikali na waasi wanaojiita Wazalendo katika mji wa Sake, umbali wa Kilomita 25 kutoka mjini mkuu wa Kivu Kaskazini Goma.

Vita hivyo vimeendelea kusababisha wasiwasi, na hata kusababisha wakaazi wa Sake kuanza kuyakimbia makaazi yao.

Ripoti za ndani zinasema, maafisa wawili wa kibinafsi kutoka Romania wanaoshrikiana na jeshi la DRC waliuawa siku ya Jumatano mjini Sake na kuwajeruhi wengine wawili.

Aidha, kwa upande jeshi la FARDC, inaripotiwa kuwa ilipoteza maafisa wake 13 na wengine 15 wakajeruhiwa huku, afisa mmoja kutoka kikosi cha SADC akijeruhiwa.

Siku ya Jumamosi, hali ya wasiwasi imeshuhudiwa kwenye eneo la Mweso Wilayani Masisi wakati huu mapigano yakiendelea kushuhudiwa.

Siku ya Ijumaa, kulikuwa na maandamano kwenye ubalozi wa Marekani na Uingereza jijini Kinshasa kwa madai kuwa, mataifa ya Magharibi yanaiunga mkono Rwanda kuendelea kuwaunga mkono waasi wa M 23, tuhuma ambazo Kigali inakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.