Pata taarifa kuu

Kenya: Jaji Mkuu afanya kikao na mkuu wa nchi

Nairobi – Jaji mkuu wa Kenya Martha Koome anafanya kikao na rais William Ruto pamoja na spika wa bunge la kitaifa kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki Moses Wetang’ula katika Ikulu ya Nairobi kwa mujibu wa taarifa ya vyombo vya habari vya ndani.

Mkuu wa nchi amekuwa akiwatuhumu baadhi ya majaji na idara ya mahakama kwa kushirikiana na upinzani kuyumbisha miradi ya serikali
Mkuu wa nchi amekuwa akiwatuhumu baadhi ya majaji na idara ya mahakama kwa kushirikiana na upinzani kuyumbisha miradi ya serikali AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

 

Jaji Mkuu katika nafasi yake kama mwenyekiti wa Tume ya kuwaajiri Majaji nchini humo (JSC) alikuwa ametaka kukutana na mkuu wa nchi kufuatia madai ya rais kuwa baadhi ya Majaji walikuwa wanajihusisha na ufisadi.

Miongoni mwa maofisa wengine wa serikali wanaohudhuria kikao hicho ni pamoja na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu, Mkuu wa Sheria Justin Muturi na wakili mkuu wa serikali Shadrack Mose kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

Tume ya kuwaajiri Majaji wiki iliyopita ilitoa wito wa kufanya kikao na rais Ruto ilikuzungumzia masuala yalioibuliwa na mkuu wa nchi kuhusu baadhi ya majaji kushirikiana na wapinzani kuhujumu miradi ya serikali yake.Mahakama ilitaka kikao na mkuu wa nchi baada ya madai kuwa baadhi ya Majaji ni wafisadi

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu Martha Koome, Tume ya kuwaajiri Majaji haitovumilia uwepo wa maofisa wake ambao ni wafisadi na kwamba iwapo madai ya mkuu wa nchi yatakuwa kweli, sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.

Chama cha mawakili nchini humo kiliandaa maandamano kulaani kile walichosema ni hatua ya mkuu wa nchi kuishambulia idara ya mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.