Pata taarifa kuu

Kigali bado ina historia ya kukosa kuheshimu haki za binadamu:London

Nairobi – Serikali ya Uingereza imekiri kwamba nchi ya Rwanda bado ina historia ya kukosa kuheshimu haki za binadamu, licha ya waziri mkuu Rishi Sunak, kusisitiza Rwanda ni salama kwa watafuta hifadhi.

Haya yanajiri wakati huu ikibainika kwamba wabunge nchini Uingereza wamegawanyika kuhusu mpango huo wa serikali kuwatuma watafutahifadhi nchini Rwanda
Haya yanajiri wakati huu ikibainika kwamba wabunge nchini Uingereza wamegawanyika kuhusu mpango huo wa serikali kuwatuma watafutahifadhi nchini Rwanda AFP - BEN BIRCHALL
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa stakabadhi kutoka kwa afisi ya waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, James Cleverly, amekiri ni kweli kwamba serikali ya Rwanda bado ina historia ya kuminya uhuru wa wanasiasa wa upinzani na uhuru wa kujieleza licha ya kwamba nchi hiyo imendelea kushuhudia amani.

Ni taarifa ilitolewa kwa bunge ili kushawishi wabunge wa Uingereza kuunga mkono juhudi za serikali kuunda sheria itakayoruhusu kuwatuma watafuta hifadhi kutoka Uingereza hadi nchini Rwanda bila kusuhudia pingamizi, baada ya mahakama ya juu kusema mpango huo ni kinyume na sheria za kimataifa za kuwalinda watafuta hifadhi.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa nchi ya Rwanda pia itahitajika kupitisha sheria mpya kuhusu watafuta hifadhi ili iwiane na mpango wa serikali ya Uingereza, ambao waziri mkuu ameufanya kuwa kipao mbele chake.

Haya yanajiri wakati huu ikibainika kwamba wabunge nchini Uingereza wamegawanyika kuhusu mpango huo wa serikali kuwatuma watafutahifadhi nchini Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.