Pata taarifa kuu

Mpaka wa Rwanda na Burundi wafungwa kufuatia mvutano wa kidiplomasia

Burundi imetangaza kufungwa kwa mipaka yake na Rwanda hivi leo, kufuatia nchi hizo jirani za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye mvutano wa kidiplomasia. 

Wanaume wakizungumza kwenye mpaka wa Burundi na Rwanda, Agosti 23, 2016.
Wanaume wakizungumza kwenye mpaka wa Burundi na Rwanda, Agosti 23, 2016. STEPHANIE AGLIETTI / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Tangazo hili limetolewa na Waziri wa usalama wa Burundi Martin Niteretse, alilolitolea katika mkoa wa Kayanza Kaskazini mwa nchi hiyo. 

Hatua hii inakuja siku chache tu baada ya rais Evariste Ndayishimiye kuishtumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa RED Tabara. 

Waasi hao wanaojificha katika mpaka na DRC mwezi Desemba mwaka uliopita, walitekeleza uvamizi kwenye ardhi ya Burundi na kuwauwa watu 20 wakiwemo watoto na wanawake. 

Rwanda inakusha madai ya Burundi. 

Hatua hii ya Burundi, imesababisha raia wa Rwanda na DRC waliokuwa wanarejea nyumbani kukwama katika mpaka wa Ruhwa, huku raia kadhaa wa Burundi waliokuwa wamevuka mpaka kwenda sokoni upande wa Rwanda wakikwama katika eneo la Bugarama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.