Pata taarifa kuu

DRC: Uamuzi kuhusu wizi wa kura unaowakabili magavana na wabunge kuamuliwa

Nairobi – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, uamuzi wa kesi ya wizi wa kura, uliowakumba wagombea wa ubunge na Magavana 82 unasubiriwa kutolewa leo au kesho.

Vyama vya upinzani vimekataa kutambua matokeo hayo ya uchaguzi wa mwaka jana
Vyama vya upinzani vimekataa kutambua matokeo hayo ya uchaguzi wa mwaka jana John WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, Baraza linalosikiliza kufutwa kwa matokeo hayo, lilitangaza kuwa, lilkuwa limepitia kesi 39 kati ya 82 na kuzifanyia maamuzi.

Matokeo hayo yalifutwa na Tume ya Uchaguzi ambayo ilidai kuwepo kwa wizi wa kura, baada ya wananchi kuwapigia kura wabunge,Magavana na Madiwani Desemba tarehe 20 mwaka uliopita.

Miongoni mwa walioathiriwa ni Mawaziri na Magavana wanaomuunga mkono rais Felix Thisekedi ambaye ushindi wake ulithibitishwa wiki hii na Mahakama ya Katiba.

Vyama vya upinzani vimekataa kutambua matokeo hayo, kwa madai ya wizi wa kura, na kuungwa mkono na waangalizi wa ndani, wakiwemo wale kutoka Kanisa Katoliki, wanaokosoa namna Tume ya Uchaguzi ilivyosimamia uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.