Pata taarifa kuu

Waomba hifadhi kutoka Libya wapokelewa nchini Rwanda

Wizara inayohusika na masuala ya dharura nchini Rwanda inasema, imewapokea waomba hifadhi 153 wakitokea nchini Libya.

Waomba hifadhi waliowasili nchini Rwanda Desemba 29 2023
Waomba hifadhi waliowasili nchini Rwanda Desemba 29 2023 © www.newtimes.co.rw
Matangazo ya kibiashara

Waomba hifadhi hao waliowasili jijini Kigali hapo jana, wanatokea katika mataifa matano.

Miongoni mwao ni raua 82 wa Sudan, 56 kutoka Eritrea, watano kutoka Somalia na tisa kutoka nchini Ethiopia, na raia mmoja wa Sudan Kusini.

Baada ya kupokewa, waomba hifadhi hao wamepelekewa katika kituo cha Gashora, Wilayani Bugesera.

Serikali nchini humo inasema hili ni kundi la 16 la waomba hifadhi iliyopokea tangu mwaka 2019, na mpaka sasa, imewapokea watu 2,059 wakati huu ikisema itaendelea kutoa huduma hiyo.

Waomba hifadhi háo wanapowasili Rwanda, huwa wanasafirishwa kwenda katika mataifa ya Ulaya na Marekani pamoja na Canada.

Sera hii ya Kigali, imeivutia Uingereza ambayo licha ya kukumbwa na kikwazo cha kisheria, kuwatuma wahamiaji haramu wanaoingia katika nchi yao nchini Rwanda, imeapa kubadilisha sheria ili kufanikisha zoezi hilo katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.