Pata taarifa kuu

Wacongomani wasubiri matokeo baada ya uchaguzi uliokumbwa na changamoto

Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa urais baada ya kupiga kura siku ya Jumatano, zoezi lililogubikwa na changamoto mbalimbali ikiwemo, watu kuchelewa kupiga kura hadi siku ya Alhamisi.

Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC CENI
Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi nchini DRC CENI REUTERS - ZOHRA BENSEMRA
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi siku ya Alhamisi ilipokea matokeo ya urais kutoka kwa Wakongamani waliopiga kura wakiwa Afrika Kusini, Ubelgiji, Ufaransa na Marekani, yaliyoonesha rais Felix Tshisekedi, anayetafuta muhula wa pili akiongoza.

CENI inasema kuanzia siku ya Jumamos , itaendelea kupokea matokeo kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, huku matokeo ya mwisho ya awali, yakitarajiwa kutangazwa tarehe 31 mwezi huu.

Zoezi la kupiga kura, lilimalizika siku ya Alhamisi katika maeneo mengi ya nchi, huku wapiga kura katika eneo la Kilembwe, Wilayani Fizi, jimboni Kivu Kusini, wakipiga kura siku ya Ijumaa.

Serikali ya Kinshasa, imekiri maeneo mengi kushuhudia ucheleweshwaji wa kufunguliwa kwa vituo na vifaa vya kupigia kura, imeisifu Tume ya uchaguzi na wapiga kura kwa kushiriki kwenye zoezi hilo.

Wapiga kura zaidi ya Milioni 44 katika nchi hiyo yenye watu zaidi ya 100, walisajiliwa kushiriki kwenye uchaguzi huo, ambao wagombea zaidi ya Laki Moja waliwania nyadhifa mbalimbali.

Katika hatua nyingine, kundi la wanasiasa wa upinzani, wamemwandikia barua, Gavana wa Kinshasa, kumpa taarifa kuwa wataanda maandamano katika jiji hili kuu wiki ijayo.

Baadhi ya wagombea urais wakiongozwa na Martin Fayulu, walilamilikia namna ucgaguzi huo ulivyofanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.