Pata taarifa kuu

DRC: WHO yawalipa waathiriwa wa kingono Dola 250 kila  mmoja

Nairobi – Shirika la afya duniani WHO, limewalipa  wanawake 104 waathiriwa  dhulma za kingono nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo fidia ya Dola 250 kila  mmoja .

Wadadisi wamehoji kiasi hicho kilicholipwa na WHO kilikuwa kidogo ikilinganishwa na gharama ya safari ya daktari Gaya ya siku tatu
Wadadisi wamehoji kiasi hicho kilicholipwa na WHO kilikuwa kidogo ikilinganishwa na gharama ya safari ya daktari Gaya ya siku tatu © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti kutoka WHO, daktari Gaya Gamhewage ,kutoka kitengo cha kupambana na dhulma za kingono,katika shirika hilo, alisafiri kwenda DRC mwezi Machi  kulishughulikia swala hilo ambapo wafanyikazi wa WHO waliokuwa wakisaidia kupambana na mlipuko wa Ebola wanatuhumiwa kuwanyanyasa kimapenzi wanawake hao 104.

Daktari Gaya katika ripoti yake kwa UN kuhusu ziara yake, amesema alikutana na wanawake hao, mmoja wao akiwa amejifungua mtoto aliyekuwa na matatizo ya kiafya na kuhitaji kugharamika zaidi kupata matibabu maalum.

WHO imesema wengi wa waathiriwa hao walikataa ofa hiyo, asilimia kubwa wakiwa hawajulikani waliko
WHO imesema wengi wa waathiriwa hao walikataa ofa hiyo, asilimia kubwa wakiwa hawajulikani waliko AP - Martial Trezzini

Wadadisi wamehoji kiasi hicho kilicholipwa na WHO kilikuwa kidogo ikilinganishwa na gharama ya safari ya daktari Gaya ya siku tatu.

WHO kabla kufanya malipo hayo,iliwasajili wanawake hao katika mafunzo ya kujifunza namna ya kujishughulisha na kupata kipato ,ingawaje wengi wa akina mama waliodhalilishwa kimapenzi waliachwa nje ,WHO ikisema wengi wao walikataa ofa hiyo, asilimia kubwa wakiwa hawajulikani waliko.

Sakata hilo la dhulma za kimapenzi ambapo wafanyikazi 83 wa WHO wanatuhumiwa kuwabaka wanawake kati ya mwaka 2018 na 2021 wakati wa Ebola,ni sakata kubwa kuwahi kuandama WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.