Pata taarifa kuu

DRC na Uganda zakubaliana kuondoa masharti ya viza kurahisisha usafiri

Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimekubaliana kuondoa masharti ya viza ili kuruhusu usafiri bila ya vyeti hivyo kati ya mataifa hayo mawili.

Makubaliano hayo yamekuja baada ya mazungumzo ya hivi karibuni kati ya maafisa wa nchi hizo mbili jijini Kinshasa
Makubaliano hayo yamekuja baada ya mazungumzo ya hivi karibuni kati ya maafisa wa nchi hizo mbili jijini Kinshasa file photo
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yanalenga kurahisisha usafiri wa watu pamoja na kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yamekuja baada ya mazungumzo ya hivi karibuni kati ya maafisa wa nchi hizo mbili jijini Kinshasa.

Kwa muda sasa, rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekuwa akishinikiza kuondolewa kwa masharti hayo kama njia moja ya kuruhusu utagamano wa watu kati ya mataifa mawili ya Afrika. 

Rais Museveni alitoa wito kwa maafisa kutoka nchi zote mbili mwezi Mei kuharakisha mchakato wa kuanzisha usafiri bila visa.

Raia wa Uganda na Kongo hapo awali wamelalamika kuhusu kulipa ada kubwa za viza katika maeneo ya mpaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.