Pata taarifa kuu

Kenya kusitisha mkataba kati yake na madaktari wa Cuba

Nairobi – Kenya itasitisha makubaliano ya miaka sita ulioruhusu zaidi ya madaktari 100 wa Cuba kufanya kazi katika hospitali za Kenya.

Mkataba wa 2017 yaliotoa nafasi kwa  madaktari wa Cuba kusaidia kujaza pengo katika hospitali za kaunti
Mkataba wa 2017 yaliotoa nafasi kwa  madaktari wa Cuba kusaidia kujaza pengo katika hospitali za kaunti © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri wa afya Susan Nakhumicha , hatua hiyo itasaidia kukabiliana na changamoto zinazowakabili wahudumu wa afya wa Kenya, ikiwemo ukosefu wa nafasi za ajira.

Mkataba wa 2017 yaliotoa nafasi kwa  madaktari wa Cuba kusaidia kujaza pengo katika hospitali za kaunti, raia wa Kenya nayo wakipata fursa ya kusafiri hadi Cuba kwa mafunzo maalum ya matibabu.

Hatua ya hiyo ya serikali ya zamani chini ya uongozi wa rais Kenyatta, ilionekana kuzua mvutano kati ya madakatari wa kenya na wale wa Cuba,  madaktari wa ndani wakieleza kuwa walikuwa na mafunzo yanayohitajika kama vile wenzao wa Cuba.

Pia kulikuwa na wasiwasi kwamba serikali ya Kenya ilikuwa ikiwalipa wataalamu wa Cuba zaidi ya wenzao wa Kenya.

Aidha mapngo huo pia ulikashifiwa na baadhi ya raia wa Kenya waliosema kuwa sehemu kubwa ya madaktari katika taifa hilo la Afrika Mashariki hawakuwa na ajira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.