Pata taarifa kuu

Uganda: Mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine amekamatwa

Nairobi – Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine, amekamatwa baada ya kurejea nyumbani akitokea kwenye ziara nje ya nchi, afisa wa ngazi ya juu wa chama amethibitisha.

Wine, mwanamzuki wa zamani ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anajulikana kama mkosoaji mkubwa wa rais Yoweri Museveni
Wine, mwanamzuki wa zamani ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anajulikana kama mkosoaji mkubwa wa rais Yoweri Museveni AP - Nicholas Bamulanzeki
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa ya David Lewis Rubongoya, katibu mkuu wa chama cha Bobi Wine National Unity Platform (NUP) katika mtandao wa X zamani ukiitwa Twitter, kiongozi wao alikamatwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege na wale anaodai kuwa ni maofisa wa serikali.

Taarifa hiyo imeambatanishwa na picha inayowaonyesha wanaume wawili wakimkamata Bobi Wine mwenye umri wa miaka 41 katika uwanja wa ndege wa Entebbe.

Mwezi uliopita, maofisa wa polisi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki walisema wamepiga marafuku mikutano iliyokuwa imepangwa na chama cha Bobi Wine
Mwezi uliopita, maofisa wa polisi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki walisema wamepiga marafuku mikutano iliyokuwa imepangwa na chama cha Bobi Wine REUTERS - ABUBAKER LUBOWA

Wafuasi wa Bobi Wine walikuwa wamepanga kuandamana naye hadi nyumbani kwake Kaskazini mwa jiji la Kampala kumkaribisha nyumbani, mkutano ambao polisi walisema ni kinyume na sheria.

Wine, mwanamzuki wa zamani ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anajulikana kama mkosoaji mkubwa wa rais Yoweri Museveni na utawala wake.

Mwezi uliopita, maofisa wa polisi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki walisema wamepiga marafuku mikutano iliyokuwa imepangwa na chama cha Bobi Wine.

Yoweri Museveni amekuwa akiongoza tangu mwaka 1986
Yoweri Museveni amekuwa akiongoza tangu mwaka 1986 © StateHouseUganda

Mwanasiasa huyo wa upinzani aliwania urais mwaka wa 2021 dhidi ya rais Museveni, ambaye amekuwa akitawala taifa hilo tangu mwaka wa 1986.

Raia wa Uganda wanatarajiwa kupiga kura kuwachagua viongozi wao wapya mwaka wa 2026, Museveni, 79, hajaweka wazi iwapo atawania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.