Pata taarifa kuu

Kenya: Miaka 10 baada ya shambulio la kigaidi katika jumba la kibiashara la Westgate

Nairobi – Leo ni miaka 10 tangu wapiganaji wa Al Shabab kuvamia jengo la kibiashara katika eneo la Westlands jijini Nairobu na kuwaua watu 67. Mashambulio hayo ya kigaidi bado ni tishio nchini Kenya.

Maofisa wa usalama nchini Kenya walikabiliana na magaidi hao kabla ya kuwazidi nguvu
Maofisa wa usalama nchini Kenya walikabiliana na magaidi hao kabla ya kuwazidi nguvu © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea jumamosi saa sita, na kudumu kwa siku nne, watu 67 wakiwauwa na wengine 200 wakijeruhiwa.

Watu wenye silaha, walivamia jengo hilo la Westgate lilokuwa na orofa nne, wakipiga risasi mfululizo na kurusha magureneti.

Kulikuwa na mashindano ya mapishi ya watoto kwenye orofa ya juu, hivyo watoto wengi walipoteza maisha.

Watu wenye silaha, walivamia jengo hilo la Westgate lilokuwa na orofa nne, wakipiga risasi mfululizo na kurusha magureneti
Watu wenye silaha, walivamia jengo hilo la Westgate lilokuwa na orofa nne, wakipiga risasi mfululizo na kurusha magureneti REUTERS/Noor Khamis

Baada ya shambulio hilo, Kenya imeshuhudia mashambulio mengine likiwemo shambulio kwenye chuo kikuu cha Garissa ambapo wanafunzi zaidi ya mia waliwauwa,shambulio la hotel ya Dusit mwaka 2019 watu 21 wakiwauwa.

Maeneo ya kaskazini mashariki na Pwani ya Kenya, haswa Lamu bado yameendelea kulengwa na Al Shabab hadi sasa, hatua ambayo imemlazimu waziri wa usalama wa ndani Kithuri Kindiki kutangaza kuwatuma vikosi maalum maeneo hayo.

‘‘Tutaweka vikosi maalum kutoka kwa maofisa wetu spesheli ambao wamepokea mafunzo maalum ya kupambana na magaidi sugu.’’ alisema waziri Kindiki.

Shambulio hilo lilitokea jumamosi saa sita, na kudumu kwa siku nne, watu 67 wakiwauwa na wengine 200 wakijeruhiwa.
Shambulio hilo lilitokea jumamosi saa sita, na kudumu kwa siku nne, watu 67 wakiwauwa na wengine 200 wakijeruhiwa. REUTERS/Thomas Mukoya

Kenya iliamua kuwatuma wanajeshi Wake nchini Somalia mwaka 2011, uamuzi ambao umeifanya kuwa shabaha ya Al Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.