Pata taarifa kuu

Mwanamume aliyehusika na mauaji sugu akamatwa Rwanda

Nchini Rwanda, mwanamume mmoja amekamatwa baada ya kubainika kuzika miili ya watu 10 ndani ya shimo moja jikoni kwake, jijini Kigali.

Maafisa wa polisi nchini Rwanda
Maafisa wa polisi nchini Rwanda AP - Muhizi Olivier
Matangazo ya kibiashara

Polisi wanasema,mwanamume huyo ana umri wa miaka 34, na amekuwa akiwatapeli watu kutoka kwenye baa na maeneo mengine ya starehe kuwapeleka nyumbani kwake na baadaye kuwauwa.

Kuna ripoti kuwa huenda idadi  ya miili iliyopatikana ni 14 kwa mujibu wa Taasisi ya taifa ya uchunguzi wa makosa ya jinai nchini humo.

Aidha, imeelezwa kuwa mshukiwa huyo alikamatwa mwezi Julai, kwa madai ya kuhusika na wizi wa mabavu, ubakaji na makosa mengine ya jinai, lakini akaachiwa kwa dhamana baada ya kukosekana kwa ushahidi dhidi yake.

Maafisa wasema, mwanamume huyo amekiri kutekeleza mauaji hayo na alipata uzoefu kwa kutazama kitendo hicho kwa wauaji sugu, na aliwatambukiza baadhi ya watu aliowauwa kwenye tindikali.

Ameeleza pia aliwanyonga, watu aliowakamata na kutumbukiza miili yao kwenye tindikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.