Pata taarifa kuu

Rais Museveni aendelea kukosoa benki ya dunia kwa kusitisha ufadhili kwa nchi yake

Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa nyengine tena amekosoa tena hatua ya benki ya dunia kwa kusitisha ufadhili kwa nchi yake, Museveni akisema hatua hiyo haitabadilisha msimamo wa raia wa taifa lake.

Rais Museveni amesema nchi yake itaendelea bila ya msaada wa benki ya dunia.
Rais Museveni amesema nchi yake itaendelea bila ya msaada wa benki ya dunia. AP - Bebeto Matthews
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwenye ukurasa wa X zamani ukijulikana kama twitter ameitaja benki ya dunia kama isiyojali.

Wiki iliyopita, benki ya dunia ilisitisha mpango wake wa ufadhili kwa taifa hilo la Afrika Mashariki kutokana na hatua ya Kampala kuidhinisha sheria inayopinga vitendo vya wapenzi wa jinsia moja mwezi Mei.

Benki ya dunia ilisema kuwa hatua hiyo ilikuwa inaenda kinuyme na kanuni zake kuhusu usawa kwa wote.

Baadhi ya mataifa ya Afrika kama vile Uganda yameharamisha mapenzi ya jinsia moja
Baadhi ya mataifa ya Afrika kama vile Uganda yameharamisha mapenzi ya jinsia moja AP

Sheria hiyo ambayo inapendekeza kufungwa jela na kutozwa faini kwa watu wanaopatikana wakiwa wanajihusisha na vitendo hivyo imekashifiwa vikali.

Museveni awali alikuwa ameikashifu benki ya dunia kwa kutumia vitisho kuishawishi Uganda kuondoa sheria hiyo na kwamba licha ya ufadili kusitishwa, nchi yake itaendelea bila ya msaada wa benki ya dunia.

Aidha rais Museveni ameeleza kuwa nchi yake inawashirika wengi wa Magahribi japokuwa wametishiwa kuhusu kuendelea kutoa msaada kwa Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.