Pata taarifa kuu

Rais Museveni ameituhumu benki kuu ya dunia kwa kutumia vitisho dhidi ya serikali yake

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ameithumu benki kuu ya dunia kwa kujaribu kutumia vitisho dhidi ya serikali yake kutokana na sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

Rais Museveni alisema kuwa Uganda itajiendeleza kwa mkopo au bila
Rais Museveni alisema kuwa Uganda itajiendeleza kwa mkopo au bila REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Tamko la rais Museveni linakuja baada ya tangazo la benki kuu ya dunia kwamba ilikuwa inasitisha mikopo yoyote mpya kwa nchi hiyo kwa misingi kwamba sheria dhidi ya mahusiano ya jinsia moja inakinzana na maadili yake.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, Rais Museveni alisema kuwa Uganda itajiendeleza kwa mkopo au bila.

Kwa mujibu wa rais Museveni, ni bahati mbaya kwamba benki ya dunia ilikuwa inawalazimisha kuacha imani, utamaduni, kanuni na uhuru wao, kwa kutumia pesa.

"Kwa kweli wanadharau Waafrika wote. Hatuhitaji shinikizo kutoka kwa mtu yeyote kujua jinsi ya kutatua matatizo katika jamii yetu. Ni matatizo yetu,” aliongeza.

Rais Museveni alitia saini sheria dhidi ya ushoga mwezi Mei, ambayo inatoa hukumu ya kifo kwa ushoga uliokithiri na kifungo cha miaka 20 jela kwa kuendeleza ushoga.

Sheria hiyo imepingwa na mashirika ya haki za binadamu nchini Uganda na kimataifa. Umoja wa Mataifa, Marekani na mataifa mengine pia yamelaani sheria hiyo mpya.

Benki ya dunia inaungana na Marekani katika kuweka vikwazo dhidi ya Uganda kutokana na sheria ya Kupinga Ushoga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.