Pata taarifa kuu

Benki ya dunia kuzuia misaada yake mipya kwa Uganda

Nairobi – Benki ya dunia, juma hili imesema itazuia misaada yake mipya kwa nchi ya Uganda, baada ya Serikali kupitisha sheria tata kuhusu watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Benki ya dunia kuzuia misaada yake mipya kwa Uganda kutokana na sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja
Benki ya dunia kuzuia misaada yake mipya kwa Uganda kutokana na sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Rais Yoweri Museveni alitia saini sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja nchini humo mwezi Mei, sheria inayotoa adhabu ya kifo kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo pamoja na kifungo cha miaka 20 jela kwa wahamasishaji wa ushoga.

Katika taarifa yake, benki ya dunia imeeleza kwamba sheria hiyo sheria hiyo inaenda kinyume na kile inachoamini kuhusu haki za binadamu.

Uganda kwa upande wake imekashifu hatua hiyo ya benki kuu ikiitaja kuwa isiyokuwa ya haki na ya kinafiki.

Benki ya dunia ilikuwa imetoa zaidi ya dolla billioni nne kwa ajili ya kufadhili maendeleo nchini Uganda mwishoni mwa mwaka wa 2022, sehemu kubwa ya fedha hizo ikielekezwa katika sekta za afya na miradi ya elimu kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Mnamo mwezi Juni, Shirika la fedha duniani (IMF) liliidhinisha kutolewa kwa dolla milioni 120 kwa nchi ya Uganda japokuwa ilionya kuhusu sheria hiyo ya kupinga mapenzi ya jinsia moja.

Kwa sasa benki kuu ya dunia imejiunga na Marekani kwa kutangaza vikwazo kwa taifa hilo la Afrika Mashariki kutokana na sheria hiyo ya kupinga mapenzi ya jinsia moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.