Kenya: Serikali kuwakabili wapiganaji wa Al-Shabaab
Nairobi – Waziri wa ulinzi nchini Kenya Adan Duale amekiiri kuwakabili kwa nguvu wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab kwenye maeneo ya mpaka wa taifa hilo la Afrika Mashariki na nchi jirani ya Somalia.
Imechapishwa:
Kauli ya waziri Duale inakuja wakati huu kasi ya mashambulio yanayotekelezwa na wapiganaji hao kwenye miji inayopakana na Somalia ikionekana kuongezeka katika siku za hivi majuzi.
Duale aidha amewaonya amesema atafanya kazi kwa ukaribu na waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki kuwanasa Wakenya wanaoshirikiana na Al-Shabaab nchini humo.
Waziri huyo ametembelea miji mitano kwenye mpaka wa Kenya-Somalia, miji ambazo zimekuwa zinakabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa kundi hilo kaskazini mashariki ya Kenya.
Viongozi kwenye maeneo hayo wametoa wito kwa jamii kushirikiana na walinda usalama katika mapambano dhidi ya Al-Shabaab.
In order to wage a successful war against terrorism and violent extremism, we must bring everyone on board. pic.twitter.com/Cg0r8P3a9P
— Hon. Aden Duale, EGH (@HonAdenDuale) July 14, 2023
Onyo la serikali ya Kenya linakuja baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa Al- Shabaab kutekeleza mashambulio kwenye maeneo matatu tofauti katika kaunti ya Mandera kaskazini Mashariki ya Kenya siku ya Ijumaa asubuhi.