Pata taarifa kuu

Uganda:  Rais Museveni amethibitisha kupona Korona

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema amepona baada ya kuambukizwa Uviko 19 mapema mwezi huu.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. AP - Bebeto Matthews
Matangazo ya kibiashara

Siku kumi na moja baada ya kiongozi huyo kuambukizwa virusi hivyo, rais Museveni amethibitisha kupona kwake kupitia ujumbe wake kwenye ukurasa wa twitter.

Rais aliweka wazi kwa umma tarehe saba ya mwezi huu kwamba alikuwa ameambukizwa Uviko 19.

 

Ametoa wito kwa raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki kufuata miendo yake ikiwemo kuepukana na uvutaji wa sigara, kufanya mazoezi pamoja kula vyakula vya kiafrika.

Kiongozi huyo amethibitisha kupona Uviko 19
Kiongozi huyo amethibitisha kupona Uviko 19 © Yoweri Museveni

Japokuwa shirika la afya duniani WHO limethibitsiha kuwa Uviko 19 sio janga tena, maambukizi hayo bado ni tishio kwa ulimwengu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.