DRC: Mjumbe wa Papa Francis amezuru Goma
NAIROBI – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Luis Antonio Tagle mjumbe maalum wa kiogozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ametembelea Goma, eneo linalokabiliwa na utovu wa usalama kutokana na mashabulizi ya mara kwa mara yanayotekelezwa na makundi ya waasi, na kuendesha misa maalum iliyoshirikisha madhebu mbalimbali, kuombea amani.
Imechapishwa:
Kwa shangwe na furaha, maelfu ya raia jijini GOMA wameishiriki Ibada hiyo iliyoongozwa na Luis Antonio Tagle , mjumbe wa Papa FRANCIS ,ambaye ametoa wito wa kuwepo kwa amani, ushirikiano pamoja na kutoa wito wa kuwepo usalama mashairki ya DRC.
“Hapa Goma tuwe pamoja , tumwe chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu , tunatoa wito wa kuwepo kwa msamaha na upatanisho na amani ya kudumu.” alisema Luis Antonio Tagle.
LUIS ANTONIO TAGLE
Baadhi ya raia wa Mji wa Goma wakristo na wasiokuwa wa Kristo walioshiriki Ibaada hiyo walizungumza na mwandishi wetu wa Goma baada ya ibaada.
“Tunamshukuru kiongozi huyo kwa kutembelea ila tunacho omba kutoka kwake ni kuzidi sana kutuombea tupate amani jimboni mwetu Kivu kaskazini.” alisema mmoja wa waliohudhuria ibaada.
Mkaazi wa Goma
Baada ya misa hiyo iliyowakusanya wakristo kutoka madhebu mbalimbali lakini pia viongozi wa Serikali na Mashirika ya kiraia , Luis Antonio Tagle anatarajiwa kuzuru kambi ya KANYARUCHINYA wilayani nyiragongo ambapo atakutana na watu waliokimbia makazi yao kutokana na mashambulio ya watu wenye silaha.
CHUBE NGOROMBI GOMA RFI KISWAHILI