Uganda: Rais Museveni azungumza wakati huu kukiwepo na uvumi kwamba amefariki
NAIROBI – Rais wa Uganda Yoweri Museveni kupitia ukurasa wake wa twitter Jumapili usiku ameandika kuwa bado anaendelea na kujitenga baada ya kuambukizwa uviko 19.
Imechapishwa:
Hatua hii ya rais Museveni, inakuja wakati huu taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa kiongozi huyo wa Afrika Mashariki amefariki baada ya kuambukizwa virusi hivyo.
Museveni aliambukiza uviko 19 tarehe saba ya mwezi Juni kabla ya rais huyo kutangaza siku moja baadae kwamba anachukua likizo kutoka kazini.
"Habari. Ni siku tano sasa tangu niambukizwe. Usiku uliopita nilala vyema nikaamka saa kumi.” kiongozi huyo alichapisha kwenye ukurasa wake wa twitter.
Ugandans, especially the Bazzukulu.
— Yoweri K Museveni (@KagutaMuseveni) June 8, 2023
Greetings. Congratulations on the Heroes’ Day of tomorrow and Congratulations on Mwalimu Nyerere’s Prayer Day (the 1st of June) and on Martyrs Day (the 3rd of June).
I congratulate the security forces for blocking all the terrorist activities…
Ametoa wito kwa raia wa Uganda kuwenda kupokea chanjo ya uviko 19 na wazee kwenda kuchomwa nyongeza ya chanjo.
Madai yameibuka kwenye mtandao wa twitter katika kipindi cha siku chache zilizopita kwamba rais Museveni alikuwa amepelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya kufariki kutokana na makali ya maambukizi ya corona.
Mwezi uliopita, shirika la afya duniani WHO mwezi jana lilitangaza kwamba maambukizi ya uviko 19 kwa sasa sio janaga la kitaifa japokuwa WHO ilionya kwamba virusi hivyo vitandelea kubadilika.