Pata taarifa kuu

Uganda: Rais Museveni ameambukizwa Uviko 19

NAIROBI – Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema ameambukizwa Uviko 19 baada ya moja ya vipimo vitatu vilivyofanyiwa uchunguzi kubainika kuwa na virusi.

Yoweri Museveni, Rais wa Uganda ameambukizwa Uviko 19
Yoweri Museveni, Rais wa Uganda ameambukizwa Uviko 19 REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Rais Museveni, ambaye alitoa hotuba yake kuhusu mustakabali wa taifa mapema Jumatano, alisema aliaanza kuhisi baridi kidogo hali ambayo ilimlazimu  kumfanyiwa kupimwa.

Katibu wa kudumu katika wizara ya afya, Diana Atwine, alisema rais amepata dalili za mafua lakini yuko katika afya njema na ataendelea na majukumu yake.

Aidha katibi huyo ameeleza kuwa rais atafuata taratibu za kudhibiti maambukizi ya uviko 19 wakati akitekeleza majukumu yake kama mkuu wa nchi.

Uganda ilikuwa mojawapo ya mataifa yaliotangaza sheria kali za kukabiliana na msambao wa maambukizi ya virusi hivyo barani Afrika, shule zikifungwa, maeneo ya kibiashara pamoja na watu kuzuiwa kutembea nje kwa muda. Nchi ilifunguliwa tena mnamo Februari 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.