Pata taarifa kuu

Rwanda: Rais Kagame amewafuta kazi maofisa wa ngazi ya juu katika jeshi

NAIROBI – Rais wa Rwanda Paul Kagame amewafuta kazi Meja Jenerali Aloys Muganga wa Jeshi la Rwanda (RDF) na Brigedia Jenerali Francis Mutiganda pamoja na wanajeshi wengine 14 wa vyeo vya juu.

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametekeleza mageuzi katika idara ya jeshi
Rais wa Rwanda Paul Kagame ametekeleza mageuzi katika idara ya jeshi © RBA
Matangazo ya kibiashara

Kati ya askari hawa 244 kwa jumla, hakuna majina yao yaliyotangazwa isipokuwa wale wawili wa cheo cha Jenerali, akiwemo Brigadia jenerali Francis Mutiganda pamoja na meja jenerali Aloys Muganga ambao wamekuwa wakihudumu katika jeshi kwa kipindi kirefu

Hii ilitokea siku moja baada ya Kagame kufanya mabadiliko makubwa katika idara ya Ujasusi kwenye jeshi la Rwanda.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Rwanda kanali Ronald Rwivanga uteuzi ulizingatia sheria, ya jeshi ina maana kwamba hawa waliofutwa kazi, wanatakiwa kukabidhi vifaa vya kijeshi na kuliacha jeshi bila faida yoyote kutokana na walichokifanya,” alisema bila kufafanua, ambapo moja wapo ni utovu wa nidhamu.

Tangazo la RDF la Jumatano wiki hii pia linasema kwamba Kagame ametoa kibali cha kuwafuta kazi wanajeshi 116 wa vyeo tofauti, na kuidhinisha kufutwa kwa kandarasi za ajira za kijeshi kwa wengine 112 wa vyeo tofauti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.